Ndege kubwa aina ya Airbus A380 mali ya Shirika la ndege la Emirates yenye uwezo wa kubeba abiria 550, imelazimika kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mkoani Dar es Salaam usiku wa Jumamosi ili kuongeza mafuta kwa ajili ya kuendelea na safari.
–
Ndege hiyo iliyobeba abiria 514 imetokea Sao Paulo, Brazil kuelekea Dubai na imelazimika kukwepa njia yake ya kawaida ya kupitia kwenye anga ya Sudan ambayo kwa sasa imefungwa kutokana na mapigano yanayoendelea.
–
Kutokana na kukwepa njia yake ya kawaida safari ya ndege hiyo imekuwa ndefu, hivyo kulazimika kutua Tanzania kwa dharura ili kuongeza mafuta yatakayoisaidia kukamilisha safari yake.