Goli la kwanza alilofunga Mshambuliaji wa Yanga SC, Fiston Mayele kwenye mchezo dhidi ya Rivers United limechaguliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) kuwa ndilo bora la wiki kati ya magoli yote yaliyofungwa mechi za raundi ya kwanza robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.