Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali za kudhibiti mapenzi ya jinsia moja nchini ikiwemo kufungia jumla ya tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagram 198, Twitter 12 na vikoa vya ‘gay’ zaidi ya 2,456.
–
“Hakuna matangazo ya mapenzi ya jinsia moja kwenye main media ambayo yanaruhusiwa, tulikuwa na changamoto kwenye online media ambapo mpaka sasa jumla ya tovuti 334, akaunti za Facebook 361, Instagrama 198, Twitter 12 zimefungiwa,” amesema Waziri Nape Nnauye.