Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Michezo ya Kubashiri M Bet, Allen Mushi afunguka kuwa wameanza rasmi kutimiza ahadi yao waliotoa pindi wameingia mkataba wa wakubaliano kuwa Mdhamini mkuu wa Klabu Simba SC iliyohusisha kutoa bonus kwa timu hio ikiwa inavuka kila hatua ya Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika.
Kwa mara ya kwanza imeanza kwa kuikabidhi klabu hio kiasi cha Tsh. Milioni 100 na kuahidi kutoa zaidi kwa hatua zijazo watakazoweza fikia katika michuano hio.
“Mwaka jana wakati tunasaini mkataba moja ya kipengele ni kutoa bonus kwa kila hatua wanayofika kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuanzia hatua ya makundi. Leo tunatoa Tsh. 100 milioni na tunawambia tu kuna zingine zitakuja.”- Mkurugenzi wa Masoko M-Bet, Allen Mushi (@mrlivinglifetz).