
Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy amesema wametekeleza maelekezo ya Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ya kuhakikisha wanatafiti vyanzo vipya vya maji vitakavyotoa huduma ya maji safi na salama yenye kutosheleza kwa wakazi wa mji wa Gairo.
“Kazi ya utambuzi wa vyanzo tumeikamilisha, tumechimba kisima cha majaribio, maji yametoka na sasa tumechukua sampuli ili kupeleka katika maabara kwa vipimo zaidi kuhusu ubora ” Mhandisi Mmasy amesema.
Kuhusu hilo, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Makame amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuamua kuleta mageuzi makubwa ya uboreshaji wa huduma za maji nchini, ikiwamo Gairo.
