
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imevitaka vituo vyote vinavyouza mafuta, kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana.
–
Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari imesema, ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei yanayoonekana vizuri kwa wateja.
–
EWURA imesema adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.