Mbunge viti maalum Mkoa wa Mara Agnes Marwa amesisitiza Serikali kuwazingatia Wachimbaji wa Madini wadogo ambao wanajitolea kwa hali na mali kujitafutia riziki ikiwa hali ya mfumo wa ajira imekuwa ni ngumu kupatikana kirahisi hapa nchini.
“Naiomba serikali iwaangalie sana wachimbaji wadogo kwa kuwa, hali ya ajira ni mbaya sana katika taifa letu, kwa kuwa wachimbaji wadogo wamejitolea na kujiajiri wenyewe basi ni vyema wakaangaliwa kwa jicho la pekee” Agnes Marwa, mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mara
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
“Kuna maeneo yamechukuliwa na wawekezaji wakubwa ambayo yamekaa muda mrefu bila kufanyiwa kazi na yamesharudishwa serikalini, ni vyema serikali ikaona namna ya kuwagawia maeneo hayo wachimbaji wadogo ili nao waweze kufaidika na ‘kasungura ka Taifa’ lao la Tanzania” Agnes Marwa, mbunge viti maalum Mkoa wa Mara
“Ni vyema yakaangaliwa maeneo yote ambayo wachimbaji wadogo wadogo wanayatumia kwa uchimbaji na yakafikishiwa umeme, hili limekuwa ni tatizo la muda mrefu hususan katika Mkoa wa Mara kwenye wanayatumia za Musoma, Bunda, Tarime. Ni vyema wachimbaji wadogo wakaangaliwa kwa jicho la pekee” Agnes Marwa, mbunge viti maalum Mkoa wa Mara