ADVERTISEMENT
Ù
Ikiwa ni utaratibu wa mara kwa mara kwa kampuni ya michezo ya ubashiri Tanzania@meridianbettz , kufikia jamii kwa kutoa kidogo wanachokipata ili kuchagiza shughuli za kimaendeleo, Wikiendi iliyopita katika kusheherekea sikukuu timu ya masoko ikiongozwa na mkuu wa kitengo cha masoko na amawasiliano cha Meridianbet Bw. Matina Nkurlu imepeleka vifaa tiba na vifaa vya usafi kwenye zahanati ya kawe jijini Dar es salaam,
Akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya hospitali hiyo, Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Daktari Isack Mbalwa amesema
“Zoezi la meridianbet kufikia na kutoa kidogo wanachokipata kwenye faida yao kurejesha kwa jamii ni zoezi la kuigwa na makampuni mengine na hasa kwenye sekta ya afya, Ukizingatia bado kwenye sekta ya afya uhitaji wake ni wa kila siku, Hivyo tuna ishukuru meridianbet na tunaomba wasituchoke”
Naye Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Meridianbet Tanzania, Matina Nkurlu alisema “ Kama ilivyo kawaida ya Meridianbet Tanzania kuikumbuka jamii yake inayomzunguka na kutoa msaada katika maeneo mbalimbali kwenye jamii kama Polisi, Vijana wa boda boda, mama lishe na katika sekta hii ya afya leo hii tumewafikia ndugu zetu wa Zahanati ya Kawe, Leo imekua bahati sana kwakua ni siku kuu na kwenye siku na zamna hii ni lazima kuwe na utaratibu wa kupeana na kwa upande wetu tumeona tutoe kidogo tulicho nacho kwa Zahanati hii. Napenda kuwahakikishia kwamba huu ni mwanzo tu wa zoezi hili sio mwisho tutarudi tena na tutaendelea kuwa karibu nanyi katika kujenga mahusiano yaliyobora zaidi”
Alisema Nkurlu ni ukweli usiopingika kwa Meridianbet Tanzania kuwa miongoni mwa makampuni makubwa nchini kwa kutoa mchango mkubwa katika sekta mbalimbali kwa kusaidia jamii.
ADVERTISEMENT