Muuguzi mwenye umri wa miaka 30 amefariki dunia baada ya kuripotiwa kujisafisha mafuta ya mwili (kupunguza uzito na nyama za tumbo) kwenye kliniki moja nchini Mexico.
–
Mwili wa mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina moja la Carina, uligunduliwa katika ofisi ya daktari bila fahamu. Inadaiwa alijaribu kuondoa mafuta kwenye sehemu yake ya kati ya tumbo, kulingana na mmiliki wa kliniki, ambaye alitoa maelezo kuhusu tukio hilo kwenye video iliyopakiwa kwenye ukurasa wake wa Facebook mnamo Machi 23.
–
Dk. Rolando Samper, mmiliki wa kliniki hiyo, alithibitisha kwamba Carina alijipa ganzi kabla ya utaratibu huo ambao haujakamilika, hata hivyo, hakuwa na aina yoyote ya mafunzo ya kuisimamia operesheni hiyo aliyokuwa anajifanyia.
–
Chombo cha habari cha eneo hilo, Presente Morelos, kinaripoti kwamba muuguzi huyo alikufa kwa ugonjwa wa moyo.