Mweka hazina wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya, Sally Bolo ameomba msamaha kwa niaba ya beki wa Simba na raia wa nchi hiyo, Joash Onyango ambaye jana alisababisha kufungwa mabao mawili katika ushindi wa Raja Casablanca 3-1 dhidi ya Simba SC nchini Morocco.
–
Sally amesema Onyango alikuwa mchezaji wa zamani wa Gor iliyokuwa inalelewa na Kiongozi wa Azimio la Umoja, Raila Odinga ambaye kwa sasa anaongoza maandamano yanayofanyika nchini humo kila siku za Jumatatu na Alhamisi hivyo imechangia Onyango kuwa na kiwango cha chini katika mechi iliyopigwa usiku wa kuamkia leo.
–
“Tunaomba Wanasimba mkubali msamaha wetu kwa niaba ya Onyango, hakukusudia kusababisha bao la kwanza na la pili. Ni hali ya game,” ameandika Sally kwenye ukurasa wa Twitter
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT