Mwanafunzi mmoja anayejulikana kwa jina la Alex Justine mwenye umri wa miaka 18 mwanafunzi wa kidato cha nne Kipaumbele Sekondari, amefariki baada ya kupigwa na radi akiwa darasani akifanya mtihani wa kujipima kwa ngazi ya Wilaya.
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo, alisema kuwa ni kweli radi limesababisha kifo cha mwanafunzi mmoja anayejulikana kwa jina la Alex Justine na wengine 44 wamejeruhiwa.
Moyo alisema kuwa jumla ya wanafunzi wa kike wamejeruhiwa na wanaendeleza vizuri huku majeruhi wa kiume wakiwa 11 huku mmoja wao akifariki kabla ya kufikishwa Hospitali ya wilaya ya Nachingwea.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu Dkt. Ramadhan Maige, alisema majira ya saa tisa na nusu alipokea simu kutoka kwa Afisa Elimu Sekondari juu ya kutokea kwa ajali iliyotokana na radi.
Dkt. Maige alisema kuwa walipokea majeruhi 45 kutoka katika shule ya sekondari Kipaumbele huku mwanafunzi mmoja akiwa tayari ameshafariki.