Rais wa Kenya, Dkt. William Ruto kama Amiri Jeshi mkuu wa Nchi hiyo amekitaka Chama cha Azimio la Umoja kuacha mchezo na kusitisha maandamano waliyopanga kufanyika Jumanne ijayo yanayoongozwa na Raila Odinga na kubainisha kuwa wakilazimisha kuandamana watajua hawajui.
–
“Nilimuita Odinga nikamuomba asitishe maandamano, wamekataa, Mimi niliwaambia ile wiki nyingine, nikaita yule Mzee wa kitendawili na nikamwambia wewe wacha hii maandamano tupeleke hii maneno yote unasema Bungeni, Wabunge waangalie kama kuna maneno ya ukweli” Rais Ruto ameyasema hayo akiwa eneo la Malava Kaunti ya Kakamega,
–
“Sasa eti wamekataa hiyo ya kwenda kuongea kwa amani Bungeni, eti wanataka kurudia maandamano, eti waende wavunje mali na kuharibu biashara ya Wananchi, Mimi ndio commander-in-chief, nyinyi mtajua hamjui, waache hiyo mchezo” ameongeza.
–
“Mambo ya uchaguzi tulimaliza last year, ile kazi imebaki sasa ni ya Viongozi, kazi imebaki ni maendeleo ya Wananchi, hakuna mali au biashara ya Wananchi itaharibika tena, Serikali ya Kenya itasimama imara kuhakikisha ya kwamba inalinda maisha na mali na biashara ya kila Mwananchi” Rais Ruto