Rivers United wameomba mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Yanga upigwe katika uwanja wao wa nyumbani, Adokiye Amaesimaka
–
Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limefanya ukaguzi wa uwanja huo baada ya kufanyiwa ukarabati na sasa wanasubiri majibu kutoka CAF
–
Rivers United hawakutumia uwanja huo katika mechi zao za hatua ya makundi baada ya kuzuiwa na CAF ukiwa umekosa vigezo
–
Mchezo wa mkondo wa kwanza kati ya Rivers United dhidi ya Yanga utapigwa Jumapili April 23 huko Nigeria na marudiano kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, April 30
–
Yanga imepania kupata ushindi wa jumla katika mechi zote mbili na kutinga nusu fainali
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT