
Rais wa Kenya William Ruto amewataka wapinzani wake kisiasa kusahau na kuachana na mazungumzo yanayohusu uchaguzi na badala yake wajikite kutetea maslahi ya wananchi.
–
Rais Ruto amesema si haki baada ya uchaguzi wanasiasa kuwarudisha nyuma wananchi kwenye masuala yanayohusu uchaguzi na viongozi.
–
Ruto amesisitiza kuwa wananchi walifanya chaguo lao katika mchakato wa kidemokrasia na walikuwa na hamu ya kuona viongozi wakitekeleza majukumu yao.
–
“Hatuwezi kuendelea kuzungumzia uchaguzi, ni wakati wa kuzungumza na kupanga mipango ya maendeleo ambayo yatabadilisha maisha ya wananchi,” alisema Rais Ruto
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT