Rais wa Kenya William Ruto amewaomba wakulima nchini humo kuongeza juhudi shambani ili kusaidia kupunguza hali ngumu ya maisha na bei za vyakula.
–
Akizungumza katika Kanisa la African Inland Church (AIC), mjini Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu wakati wa ibada ya Jumapili Aprili 9, Ruto amesema anafahamu ukweli kwamba Wakenya wengi wanateseka kutokana na gharama ya juu ya maisha na bei ya vyakula.
–
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Ameongeza kuwa serikali yake inafanya kila iwezalo kubadili hali hiyo akibainisha kuwa kuanzia wiki ijayo bei zitashuka.