Mchezo wa jana Simba kuna kitu walijaribu kukionyesha lakini changamoto kwao ni makosa yaliyofanyika kwenye safu ya ulinzi.
–
Pindi unapokutana na timu kubwa kama Raja Casablanca yenye wachezaji wakubwa kama wakina Amza Khaba lazima watatumia makosa yakoo kwa ufasaha watafunga mabao.
–
Simba SC wanaelekea hatua ya robo fainali hatua ambayo unakutana na timu nyinga zenye uwezo kama Raja ama zaidi ukifanya makosa kama yale utakuwa unajiweka kwenye wakati mgumu.
–
Mwalimu Robertinho anatakiwa kuja na mpango wa muda mfupi kuiandaa timu yake kwenye michezo mikubwa inayofwata ajaribu kuangalia namna ambavyo safu ya ulinzi inaweza kupunguza makosa.
–
Pia anatakiwa kuwa na mpango wa muda mrefu kwa maana ya kuanza kufwatilia mchezaji mwenye uwezo mkubwa na ataongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi.
–
Credit : Kessy Sport Tz