Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Sheikh Nuhu Mruma amesema, sikukuu ya Eid El – Fitri itakuwa kati ya Aprili 21 au 22 kutegemea mwandamo wa mwezi. Amesema sherehe za Eid El – Fitri kitaifa mwaka huu zitafanyika mkoani Dar es Salaam.
–
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Swala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohammed VI, BAKWATA makao makuu Kinondoni. Sheikh Mruma ameeleza hayo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari kuhusu mwenendo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na uwezekano wa siku itakayosherehekewa sikukuu ya Eid.