Simba Queens imeifunga timu ya Mkwawa Queens magoli 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Wanawake #SLWPL uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru,Dar es Salaam.
–
Magoli ya Simba katika mchezo huo yamefungwa na Jentrix Shikangwa aliyefunga magoli mawili dakika ya 19′ na dakika ya 31′ , Vivian Corazone dakika ya 80′ na Zainabu Mohamed dakika 90+.
–
Mara baada ya kufunga magoli mawili katika mchezo wa leo mshambuliaji wa Simba Queeens, Jeatrix Shikangwa anafikisha idadi ya magoli 13 hadi hasa, Wakati Simba Queens wakikwea hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Wanawake #SLWPL wakiwa na alama 33 katika michezo 14 waliocheza mpaka sasa.
–
Ni tofauti ya alama mbili tu na Jkt Queens waliopo nafasi ya pili wenye alama 31 wakiwa na mchezo mmoja mkono.