Steven Gerrard yupo kwenye orodha ya makocha wanaofatiliwa na klabu ya Olympiakos ya Ugiriki ili kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa muda mfupi (miezi sita).
–
Gerrard (42) amekuwa hana kazi tangu alipofutwa kazi na Aston Villa Oktoba 2022, ambayo aliingoza katika mechi 39, akishinda mechi 12, sare 8 na vipigo 19. chini ya usimaizo wake yake klabu hiyo ilifunga magoli 45 na kuruhusu kufungwa magoli 53.
–
Lakini Sport-FM ya Ugiriki inasema kuwa Gerrard sio chaguo bora kwa klabu ya Olympiakos, badala yake, wafanye mpango wa kumnasa Gennaro Gattuso, kiungo wa zamani wa AC Milan.
–
Gattuso na Gerrard wana historia, Gerrard alishinda fainali ya Ligi ya Mabingwa 2005 na Gattuso akilipiza kisasi katika fainali mwaka 2007.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Related
Tags: Steven Gerrard