Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanaendelea vyema huku akitoa takwimu zinazoonesha kuwa kwa mwaka 2022 jumla ya tani 20.6 za bangi zilikamatwa katika maeneo mbalimbali nchini.
–
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Akizungumza katika siku ya uzinduzi wa mbio za mwenge kitaifa mjini Mtwara amesema mashamba yenye jumla ya ekari 21 ya Bangi yametekezwa kwa mwaka 2022, huku Mirungi tani 15 ikikamatwa na dawa za kulevya aina ya Heroine kilo 255 zikikamatwa pia.