
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limesema uchumi wa Tanzania umekuwa kwa kasi na kuyazidi baadhi ya mataifa ya Ulaya ikiwemo Croatia, Lithuania, Serbia na Slovenia.
–
Kwa mujibu wa takwimu za shirika hilo pato la taifa la Tanzania limeongezeka kufikia Dola za Marekani Bilioni 85.42 (Shilingi Trilioni 200) kwa mwaka huu wa 2023.
–
IMF imeongeza kuwa mafanikio hayo yamechangiwa na sera za uchumi zilizoongeza uwekezaji na kujenga tija kwenye uchumi.
–
IMF imetabiri ongezeko la pato hilo la taifa kwa Tanzania hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 136.09 (Sh. Trilioni 276) ifikapo mwaka 2028.
–
Wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani mwaka 2021 pato la taifa kwa Tanzania lilikuwa Dola za Marekani Bilioni 69.9 (Shilingi Trilioni 163.5) na amekuwa akisisitiza mageuzi ya kisekta katika kuimarisha uchumi ikiwemo sera ya kuifungua nchi.