Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema mifumo ya malipo ipo imara, huku akidai waliohusika kuongeza fedha za manunuzi ya ndege hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
–
Dk Mwigulu ametoa kauli hiyo bungeni leo April 6,2023 wakati akimpa taarifa Mbunge wa Viti Maalum, Ester Matiko alipokuwa akichangia bungeni mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2023-2024.
–
Katika mchango wake Matiko amedai kuna ubadhilifu mkubwa katika ununuzi wa ndege huku wahusika wakikaa kimya bila kusema jambo lolote.