Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla, ametangaza Kuanza kwa operesheni kabambe ya kukamata wazalishaji na Watumiaji wa Mifuko ya ‘plastiki’ iliyokatazwa, kuanzia Mei Mosi ambapo amewataka Wananchi kuanza kuchukuwa tahadhari.
–
RC Makalla, ameelekeza Baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC kwa kushirikiana na TBS, kuweka ratiba ya Siku za kutoa elimu kwenye Wilaya zote za Mkoa huo, kabla ya Kuanza kwa operesheni hiyo Ili kujenga uelewa.
Hatua hiyo imekuja, baada ya matumizi ya mifuko ya plastic iliyokatazwa Kuanza kurudi upya, Licha ya Serikali kupiga marufuku.
–
Akizungumzia wakati wa mkutano wa udhibiti mifuko ya plastic, Kelele za mziki na mitetemo, Makalla pia amewataka Wamiliki wa Bar, Kumbi za starehe na Vyombo vya mzikibkufuata na kuzingatia Sheria, Kanuni na miongozo NEMC ili kuepusha kero ya Kelele za mziki kwa Wananchi.
–
Katika mkutano huo uliohusisha Viongozi wa mitaa, Masoko na wadau wa mazingira, ameelekeza Viongozi wa Serikali za mitaa kuchukuwa hatua ikiwa ni pamoja na kudhibiti utoaji vibali vya ujenzi kiholela.