Mkurugenzi wa Mashtaka ya umma nchini Uganda jana aliidhinisha Mashtaka ya ufisadi dhidi ya Waziri wa Masuala ya Karamoja Bi.Mary Goretti Kitutu kwa kuhusika na kashfa ya wizi wa mali ya umma.
–
Mashtaka hayo ni ya rushwa na kula njama kutenda uhalifu juu ya mabati yaliyokusudiwa kwa ajili ya mpango wa uwezeshaji wa waathirika wa majanga katika mkoa wa Karamoja.
–
Spika wa Bunge la Uganda, baadhi ya wabunge pamoja na kaka wa Waziri huyo nao walitajwa katika kashfa hiyo iliyohusisha wizi wa mabati zaidi ya 5,500.
–
Waziri Kitutu ambaye alikuwa akishikiliwa na polisi tangu juzi alifikishwa katika Mahakama ya kupambana na rushwa leo, yeye pamoja na kaka yake Michael Kitutu wamefunguliwa mashtaka.
–
Wawili hao walinyimwa dhamana hivyo wamepelekwa rumande na kesi yao itasikilizwa tena baada ya sikukuu za Pasaka.
–
Rais Yoweri Museveni ametoa wito wa kufunguliwa mashtaka kwa wale wote watakaokutwa na hatia.