Afisa Mtendaji Mkuu wa Yanga SC, Andre Mtine amesema timu hiyo inahitaji ushindi dhidi ya TP Mazembe ili kuongoza kundi lao.
–
Mtine amedai kuwa mchezo wao wa kwanza na Mazembe walihitaji kushinda ili kufuzu lakini pia kutuma salamu kwenye ramani ya soka la Afrika.
–
”Tunahitaji kuifunga TP Mazembe kwa sababu tunahitaji kuongoza kundi, najua haitakuwa rahisi lakini lazima tushinde.”
–
”Katika mchezo wa kwanza tulihitaji kuwafunga TP Mazembe sababu tulihitaji kufuzu lakini pia kutuma salamu na hakika salamu tulituma baada ya kuwafunga.”
–
Yanga itashuka uwanjani kesho siku ya Jumapili majira ya saa 10:00 jioni kumkabili mwenyeji wake TP Mazembe huku timu hiyo ya Congo ikiwa tayari imeshatupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya Young Afrika kuongoza kundi kwa alama 10 na nafasi ya pili ikichukuliwa na US Monastir wenye pointi 10.