Mahakama ya Mkoa Vuga leo, Mei 15, 2023 imemuhukumu mshtakiwa Jamal Ali Geto mwenye umri wa miaka 23 kutumikia kifungo cha miaka 30 katika Chuo cha Mafunzo na kulipa fidia ya shilingi 500,000 kwa kosa la kubaka.
–
Akisoma maelezo ya huku hiyo Hakimu wa Mahakama hiyo Taki Abdalla Habibu amesema Mahakama imejiridhisha na Ushahidi uliotolewa Mahakamani na kumtia hatiani mutuhumiwa kwa kosa hilo.
–
Awali Mshtakiwa huyo alishatakiwa kwa kosa la kubaka kinyume na kifungu namba 108(1)(2)e na 109(1) cha sheria namba 6/2018.
–
Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakamani hapo Novemba 02, 2022 na jumla ya mashahidi sita (6) walitoa Ushahidi wao Mahakamani na kusomwa hukumu hiyo leo.