ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, June 5, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

BANDARI YA DAR ES SALAAM YAIPIKU MOMBASA KATIKA ORODHA MPYA YA BENKI YA DUNIA

Dar es Salaam

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
May 25, 2023
in HABARI
0
BANDARI YA DAR ES SALAAM YAIPIKU MOMBASA KATIKA ORODHA MPYA YA BENKI YA DUNIA
0
SHARES
21
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

TICTS Maintains Record Productivity - TanzaniaBandari za Dar es Salaam, Djibouti na Berbera zimeipita Mombasa katika orodha ya hivi punde ya Benki ya Dunia kwenye bandari zenye ufanisi zaidi, ikionyesha hofu ya ushindani ambayo Kenya imekuwa nayo juu ya Tanzania kuwa njia inayopendelewa kwa wasafirishaji.

Toleo la tatu la Matokeo ya Utendaji kazi wa Bandari ya Kontena duniani limeweka bandari ya Mombasa katika nafasi ya 326 mwaka wa 2022 kati ya bandari 348 duniani kote ambazo zilitathminiwa, nyuma ya bandari hizo za Afrika mashariki.

RelatedPosts

SIMBA SC IMEWAHI KUCHEZA FAINALI CAF 1993

SIMBA SC IMEWAHI KUCHEZA FAINALI CAF 1993

Jun 5, 2023

KARIM BENZEMA KUONDOKA RASMI MADRID BAADA YA KUICHEZEA KWA MISIMU 14, BERNABEU

Jun 4, 2023

2023 Middle East Analyst Program, EMEA, Full Time Analyst Job Vacancy at citi Bank

Jun 4, 2023
Load More

Bandari kuu ya Kenya ilirekodi kushuka kwa kasi kutoka kwa ripoti ya 2021 ambapo iliwekwa katika nafasi ya 296 na Benki ya Dunia.

Bandari hizo zimeorodheshwa kulingana na ufanisi wao, unaopimwa na muda uliopita kati ya wakati meli inafika bandarini hadi kuondoka kutoka kwenye kituo ikiwa imekamilisha kubadilishana mizigo.

Benki ya Dunia inabainisha kuwa uendeshaji mzuri wa bandari hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya biashara katika eneo hilo, ikisema kuwa kumekuwa na uboreshaji mkubwa katika biashara tangu 2020 wakati sekta ya usafiri wa baharini ilirekodi shughuli zilizopunguzwa kutokana na janga la Covid-19.

“Kuboresha ufanisi wa bandari ni muhimu kwa kufungua ukuaji na maendeleo ya Afrika,” alisema Martin Humphreys, mwanauchumi mkuu wa usafiri katika Benki ya Dunia.

“Bandari za Afrika ni lango muhimu kwa biashara na uendeshaji bora unachangia usalama wa chakula. Uendeshaji wao wenye ufanisi ni kigezo muhimu cha kuamua ikiwa Afrika itafikia uwezo wake wa kiuchumi.”

Haya yanajiri wakati Bandari ya Dar es Salaam ya Tanzania katika miaka ya hivi karibuni imekuwa na ushindani mkubwa, na kutishia kuvuta meli nyingi zinazoingia katika bahari ya Afrika Mashariki kwenye bandari yao.

Katika orodha hiyo, bandari ya Tanzania ilirekodi kuimarika kutoka nafasi ya 2021 hadi kushika nafasi ya 312 kutoka 361 ya awali.

Takwimu kutoka Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) zinaonyesha kiasi cha mizigo inayohudumiwa na bandari ya Mombasa kilishuka kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano mwaka wa 2022, huku wadau wakiashiria kuongezeka kwa ushindani kutoka Dar es Salaam.

ADVERTISEMENT

Jumla ya shehena ya mizigo bandarini ilipungua hadi tani milioni 33.74 mwaka jana kutoka tani milioni 34.76 mwaka uliopita, kulingana na KNBS.

Kushuka kwa asilimia 2.93 kwa mwaka kulifanya idadi hiyo kuwa ya chini kabisa tangu 2018 ilipofikia tani milioni 30.92.

ADVERTISEMENT

Source Cc; BBC Swahili

Related

Tags: BANDARI YA DAR ES SALAAMBENKI YA DUNIADar es SalaamNICWIZARA YA BIASHARAWIZARA YA BIASHARA NA UWEKEZAJIWORLD BANK
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

WAZIRI MCHENGERWA ATOA OFA HII BABU KUBWA KUIPONGEZA YANGA
HABARI

WAZIRI MCHENGERWA ATOA OFA HII BABU KUBWA KUIPONGEZA YANGA

by ALFRED MTEWELE
Jun 5, 2023
MAKAMU WA RAIS AONGOZA ZOEZI LA USAFI SOKO LA MACHINGA DODOMA, NEMC YAACHIWA MAAGIZO HAYA
HABARI

MAKAMU WA RAIS AONGOZA ZOEZI LA USAFI SOKO LA MACHINGA DODOMA, NEMC YAACHIWA MAAGIZO HAYA

by ALFRED MTEWELE
Jun 5, 2023
KUNANI MAGAZETINI LEO JUMANNE TAREHE 22 JUNI
HABARI

KURASA ZA MAGAZETINI LEO JUMATATU TAREHE 05 JUNI 2023

by I am Krantz
Jun 5, 2023
UJUE MPANGO MPYA WA VITUO VYA KUCHAJI MAGARI YA UMEME NCHINI
HABARI

UJUE MPANGO MPYA WA VITUO VYA KUCHAJI MAGARI YA UMEME NCHINI

by ALFRED MTEWELE
Jun 4, 2023
Rais Samia Apunguza Tozo Ya Mafuta
HABARI

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan awaalika Yanga kwa chakula cha jioni kesho Jumatatu

by I am Krantz
Jun 4, 2023
166 New Job Vacancies at TANAPA
HABARI

166 New Job Vacancies at TANAPA

by ALFRED MTEWELE
Jun 4, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2023
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In