ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, June 2, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Benki ya NBC yazindua huduma ya NBC Connect Kanda ya Ziwa

I am Krantz by I am Krantz
May 20, 2023
in HABARI
0
Benki ya NBC yazindua huduma ya NBC Connect Kanda ya Ziwa
0
SHARES
30
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 2, 2023

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 2, 2023

Jun 2, 2023

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2bn/-

Jun 2, 2023

SERIKALI YAPOKEA BILIONI 15 KUTOKA UINGEREZA KWAAJILI YA MPANGO WA TASAF

Jun 1, 2023
Load More
.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bulandya Elikana, akizungumza na wateja wa benki ya NBC wakati wa kuzindua huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Mkuu wa kwa Kitengo cha Wateja wa Kimataifa wa NBC Wilson Nkuzi, akizungumza na wateja wakati wa uzinduzi wa huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Mkuu wa Kitengo cha Kidigitali na Miamala wa benki ya NBC Jimmy Myalize, akiwasilisha mada ya namna ya kufanya miamala kwa njia nafuu na rahisi wakati wa uzinduzi huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Baadhi ya wateja wa benki ya NBC na wadau wa sekta ya fedha wakipiga makofi kuipongeza benki hiyo, wakati wa kuzindua huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bulandya Elikana (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Kimataifa wa benki ya NBC Wilson Nkuzi wakati wa kuzindua huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Baadhi ya wateja wa benki ya NBC na wadau wa sekta ya fedha wakifuatilia hotuba na mada mbalimbali, wakati wa uzinduzi wa huduma ya NBC Connect kwa kanda ya Ziwa, katika hafla iliyofanyika jijini Mwanza.

Mwanza Mei 19, 2023:  Makampuni pamoja na taasisi mbali mbali  ambazo ni wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara ya (NBC), sasa wanaweza kupata uzoefu mpya wa huduma za kibenki kupitia huduma ya NBC Connect, ikiwa ni ingizo jipya la huduma za kibunifu za kidigitali.

NBC Connect, ni huduma ya kisasa ya kidigitali, ambayo huwezesha huduma salama za kibenki ambazo huweza kufanyika sehemu yoyote, muda wowote kwa njia ya mtandao. Huduma hii ni sehemu ya mchango wa benki katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuongeza ujumuifu katika huduma za kifedha (financial inclusion)

Uzinduzi wa huduma ya NBC Connect kanda ya Ziwa, ni wa pili baada ya uzinduzi kwa kanda ya nyanda za juu kusini uliofanyika jijini Mbeya mwezi uliopita.

Kupitia NBC Connect, wateja wenye makampuni na taasisi mbali mbali zilizopo mkoa wa Mwanza na maeneo ya  jirani, watapata fursa na uwezo wa kufanya miamala yao ya kifedha kwa urahisi zaidi na kupata uzoefu  mpya katika kupata huduma za kibenki.

Huduma itawapa wateja uwezo wa kufanya miamala kirahisi ikiwa ni pamoja na malipo ya ndani na nje ya nchi, malipo ya Serikali pamoja na malipo kwa mkupuo bila kuchukuas muda kwa kutumia simu au kompyuta. Wateja pia wataweza kupata taarifa za miamala waliyofanya popote pale walipo pasipo kulazimika kwenda benki.

NBC Connect imetengenezwa kwa teknalojia ya kisasa na yenye usalama wa hali ya juu ambayo imezingatia na kutoa kipaumbele kwenye usiri wa taarifa za mteja. Ubunifu wa huduma hiyo huakikisha taarifa za kifedha za wateja zinalindwa wakati wote.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, mkuu wa kitengo cha wateja wa kimataifa wa benki ya NBC Wilson Nkuzi , “Tunafuraha kutambulisha NBC Connect kwa wakazi wa kanda ya ziwa na maeneo ya jirani. Mfumo huu wa kibenki wa kidigitali ni uthibitisho wa dhamira ya kuwapatia wateja wetu huduma  bora za kibenki ambazo ni rahisi, salama, na zinazofaa na kukidhi mahitaji ya wateja. NBC Connect itawawezesha wateja wetu kufanya huduma zakibenki popote pale, wakati wowote, na kufurahia huduma hizo bila matatizo.”

Pamoja na huduma rahisi na za kisasa, NBC Connect itatoa usaidizi wa binafsi kwa wateja kupitia kituo chake cha huduma kwa wateja ambapo mameneja wetu katika kituo cha huduma kwa wateja wanapatikana ili kuwasaidia wateja kulingana na mahitaji yao nakutoa mwongozo wa jinsi ya kutumia jukwaa hilo kwa ufanisi.

Ili kusherehekea uzinduzi wahuduma hiyo jijni Mwanza, Benki ya NBC itatoa maelezo ya kina juu ya huduma hiyo na  kwa wateja watakaojiandikisha na kujiunga na huduma hiyo ili kuwapa uelewa mpana wa namna ya kuitumia na kufurahia huduma hiyo.

“Tunawaalika wateja wetu wote wa kanda ya Ziwa na maeneo ya jirani  wajionee urahisi na usalama wa NBC Connect. Ni huduma ambayo inaleta mapinduzi mapya katika namna ambavyo huduma za kibenki zinatolewa. Tuna uhakika  kuwa wateja wetu watafaidika nayo kwa kiasi kikubwa , “aliongeza

ADVERTISEMENT

Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Mwanza Bulandya Elikana aliishukuru Benki ya NBC kwa ubunifu wao mzuri na kuwahimiza wateja kutumia mfumo huo mpya wa kibenki ili kurahisisha shughuli zao za kila siku.

“Uzinduzi wa NBC Connect kanda ya Ziwa unawakilisha mpango mkakati wa upanuzi wa benki ya NBC ili kuwafikia wananchi wengi zaidi  na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi. Benki ya NBC inasifika kwa dhamira yake kubwa ya kuwajibika kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kusaidia jamii kupitia mipango mbalimbali, kama vile Mbio za Kimataifa za NBC Dodoma Marathon zinazohamasisha matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi, msaada wa afya ya uzazi kupitia kliniki zinazotembea, programu za elimu ya kifedha, uwezeshaji wa vijana. kupitia udhamini wa Ligi Kuu ya NBC, hakika napongeza juhudi hizi zinazofanywa na NBC” alisema

 

MWISHO……….

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 2, 2023
HABARI

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 2, 2023

by ALFRED MTEWELE
Jun 2, 2023
Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2bn/-
HABARI

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2bn/-

by I am Krantz
Jun 2, 2023
SERIKALI YAPOKEA BILIONI 15 KUTOKA UINGEREZA KWAAJILI YA MPANGO WA TASAF
HABARI

SERIKALI YAPOKEA BILIONI 15 KUTOKA UINGEREZA KWAAJILI YA MPANGO WA TASAF

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023
RAIS DK. MWINYI AZINDUA KAMATI YA KUZUIA UDHALILISHAJI ZANZIBAR
HABARI

RAIS DK. MWINYI AZINDUA KAMATI YA KUZUIA UDHALILISHAJI ZANZIBAR

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023
WANAWAKE WAONYWA UNYANYASAJI DHIDI YA WANAUME
HABARI

WANAWAKE WAONYWA UNYANYASAJI DHIDI YA WANAUME

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023
JINSI YA KUSAJILI BIASHARA YAKO
HABARI

JINSI YA KUSAJILI BIASHARA YAKO

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2023
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In