ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, June 5, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

BUNIFU ZETU ZIENDE SOKO LA KIMATAIFA

Dar es Salaam

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
May 24, 2023
in HABARI
0
BUNIFU ZETU ZIENDE SOKO LA KIMATAIFA
0
SHARES
24
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

No alt text provided for this imageInaelezwa kuwa, wabunifu wa Tanzania ni wazuri lakini wanahitaji kutangazwa ili waonekane na watu wenye kampuni kubwa duniani waweze kuwekeza katika uzalishaji.

Hayo yanaelezwa na Meneja Usimamizi na Uhawilishaji Teknolojia kutoka Tume ya Sayansi na Teknojojia (COSTECH), Erasto Mlyuka katika ufunguzi wa semina ya siku tatu inayofanyika katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa watumishi 45 wa DIT ili kuwajengea uwezo na kuimarisha vituo vya teknolojia na ubunifu.

RelatedPosts

SIMBA SC IMEWAHI KUCHEZA FAINALI CAF 1993

SIMBA SC IMEWAHI KUCHEZA FAINALI CAF 1993

Jun 5, 2023

KARIM BENZEMA KUONDOKA RASMI MADRID BAADA YA KUICHEZEA KWA MISIMU 14, BERNABEU

Jun 4, 2023

2023 Middle East Analyst Program, EMEA, Full Time Analyst Job Vacancy at citi Bank

Jun 4, 2023
Load More

“Wabunifu wetu Tanzania ni wazuri lakini wanahitaji kutangazwa ili watu wenye fedha, wenye kampuni kubwa duniani waje kuwekeza kwenye bunifu zao,” anasema Erasto na kuwataka vijana kuwa na utamaduni wa kushirikiana na si kushindana katika ushindani wa kimataifa.

“Kama ni kushindana kuwe ni kwa tija, kama mbunifu mmoja ana kitu cha kipekee na mwingine ana kitu cha kipekee mnaweza kuja pamoja na kupata mtaji kufanya kitu pamoja,” amesema.

Hata hivyo Erasto amesema nchi iko mahali pazuri kwani kwa mujibu wa takwimu za ripoti ya mwaka huu kuna kampuni changa zaidi ya 600, amesema “tunaamini kila kampuni inapambana kuhakikisha inapata mtaji ili bunifu ziwafikie walaji na tunaamini tutaendelea kuonekana kimataifa.”

ADVERTISEMENT

Mratibu wa Utafiti, Ubunifu na Machapisho wa DIT, Dkt. Daudi Simbeye amesema semina hiyo ina lengo la kuboresha utafiti na bunifu zisiweze kuibuwa au kuzalishwa na watu wengine ndani na nje ya nchi, kupitia semina hiyo iliyoratibiwa kwa kushirikiana na COSTECH, walimu na wanafunzi wataweza kulinda bunifu zao.

“Hapa kwetu DIT tumejikita zaidi katika kufundisha na kutoa ushauri wa kitaalam, pia tumekua tukifanya bunifu mbalimbali lakini changamoto ni namna gani ya kulinda bunifu zetu, semina hii inakwenda kutuongoza nini cha kufanya katika changamoto hiyo,” amesema.

“Moja ya faida ya semina hii ni kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa ikiwa ni zile zinazotokana na bunifu zetu ziweze kuwa bora na zishindane kitaifa na kimataifa na ziweze kuleta tija na kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,” amesema Dkt. Simbeye.

Ameshauri serikali kuendelea kuzipa taasisi vifaa vya kufundishia vya kutosha na vya kisasa ili ziendelee kuzalisha vijana wenye tija na taasisi hizo ziendee kusaidia kutatua changamoto katika jamii.

Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia dar es Salaam, Prof. Preksedis Ndomba amepongeza COSTECH kuendesha mafunzo hayo ambayo yatasaidia wabunifu kunufaika na bunifu zao.

“Ni matarajio yangu baada ya semina hii wataalamu wetu watakuja na mpango kazi bora wa kubiasharisha bunifu zetu lakini pia bunifu na teknolojia nyingi zaidi zitabiasharishwa,” amesema Prof. Ndomba.No alt text provided for this imageNo alt text provided for this image

ADVERTISEMENT

 

 

Related

Tags: BUNIFUDar es SalaamDITNMB BANKSOKO LA KIMATAIFAUNITED REPUBLIC OF TANZANIAWIKI YA UBUNIFU
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

WAZIRI MCHENGERWA ATOA OFA HII BABU KUBWA KUIPONGEZA YANGA
HABARI

WAZIRI MCHENGERWA ATOA OFA HII BABU KUBWA KUIPONGEZA YANGA

by ALFRED MTEWELE
Jun 5, 2023
MAKAMU WA RAIS AONGOZA ZOEZI LA USAFI SOKO LA MACHINGA DODOMA, NEMC YAACHIWA MAAGIZO HAYA
HABARI

MAKAMU WA RAIS AONGOZA ZOEZI LA USAFI SOKO LA MACHINGA DODOMA, NEMC YAACHIWA MAAGIZO HAYA

by ALFRED MTEWELE
Jun 5, 2023
KUNANI MAGAZETINI LEO JUMANNE TAREHE 22 JUNI
HABARI

KURASA ZA MAGAZETINI LEO JUMATATU TAREHE 05 JUNI 2023

by I am Krantz
Jun 5, 2023
UJUE MPANGO MPYA WA VITUO VYA KUCHAJI MAGARI YA UMEME NCHINI
HABARI

UJUE MPANGO MPYA WA VITUO VYA KUCHAJI MAGARI YA UMEME NCHINI

by ALFRED MTEWELE
Jun 4, 2023
Rais Samia Apunguza Tozo Ya Mafuta
HABARI

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan awaalika Yanga kwa chakula cha jioni kesho Jumatatu

by I am Krantz
Jun 4, 2023
166 New Job Vacancies at TANAPA
HABARI

166 New Job Vacancies at TANAPA

by ALFRED MTEWELE
Jun 4, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2023
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In