Klabu ya Manchester United ikiwa ndio mwenyeji wa mchuano iliichapa goli 4-1 Chelsea katika mchezo huo uliochezwa hapo jana na kufanya Chelsea iendelee kutoka kabisa kwenye rekodi ya kushinda michuano hio mfululizo kama ilivyozoeleka kwa klabu hio hapo awali.
Kwa mwelekeo huo Wadau na Mashabiki wa klabu hio wanaona Chelsea inazidi potea katika mfumo wa umiliki wa kusakata ikandanda vilivyo kwani haijawa na uhakika wa kupata matokeo mazuri katika mechi zaidi ya 3 au tano mfululizo.
Kushindwa kwa klabu hio kufanya vizuri kunaendelea kuwapotezea matumaini wafuasi wake katika kuiona timu yao kusalia nafasi nzuri Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa msimu ujao ambapo Man City, Arsenal na Man United wamekuwa wakijitahidi kujikita zaidi katika nafasi za juu kama miamba ya soka ya Ligi hio ya EPL.