Daktari wa Familia ya aliyekuwa Mwanadiplomasia na Mtaalamu wa Masuala ya Mahusiano ya Kimataifa na Usalama, Mbunge kwa Miaka 15 na Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, Prof. Harun Nyagori ametoa sababu iliyopelekea kifo cha Mwanadiplomasia huyo.
Dkt. Nyagori amesema Membe amekuwa ni mtu mwenye afya njema wala sio wa kusema amewahi sumbuliwa na magonjwa sugu ila siku tatu nyuma alipatwa na tatizo la kubanwa nakifua ambacho kilikuwa cha ghafla ambapo jana alizidiwa ghafla na kupelekea complications hadi kushindwa kupumua, hali hio imepelekea kufariki.
Aidha aliongezea kuwa hali aliyokuwa nayo ilikuwa ni ya kawaida hauuwezi kuchukulia kitu serious sana maana kulingana na hali ya sasa maradhi kama hayo humpata mtu yeyote.
Daktari Prof. Nyagori amesema kifo cha Bernard Membe ni cha kawaida tu na wala sio kama vile mawazo potofu yanayotolewa kutaja kwamba ameuwawa au amepatiwa sumu, hizo ni taarifa za kupuuzwa.