ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, June 10, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

HUDUMA YA NBC CONNECT YAZINDULIWA MBEYA ,KUBORESHA HUDUMA ZA KIBENKI MKOANI HUMO

I am Krantz by I am Krantz
May 1, 2023
in HABARI
0
HUDUMA YA NBC CONNECT YAZINDULIWA MBEYA ,KUBORESHA HUDUMA ZA KIBENKI MKOANI HUMO
0
SHARES
255
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

Mkurugenzi wa Kitengo cha wateja Wakubwa wa benki ya NBC Bw. James Meitaron (wa kwanza kulia ) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa ( wa Pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Bw. Elvis Ndunguru (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dr.Kassim Hussein wakati wa uzinduzi wa NBC Connect , jukwaa la kidigitali la kisasa linalotoa huduma za benki kwa urahisi na salama, wkwa kutumia simu na vifaa vinavyotumia mtandao (Intaneti ).. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Mbeya.

 

RelatedPosts

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI MPYA YA SHINDA MECHI ZAKO NA NBC

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI MPYA YA SHINDA MECHI ZAKO NA NBC

May 3, 2023

NAFASI ZA KAZI BENKI YA NBC

Apr 25, 2023

NBC YASHIRIKI UWEKAJI WA  JIWE LA MSINGI  UJENZI WA RELI YA KISASA (SGR) KIPANDE CHA NNE TABORA – ISAKA

Jan 20, 2023
Load More

 

 

ADVERTISEMENT
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa akitoa hotuba kwa wageni waalikwa (hawapo pichani )wakati wa uzinduzi wa NBC Connect , jukwaa la kidigitali la kisasa linalotoa huduma za benki kwa urahisi na salama, wakati wowote na mahali popote kwa kutumia simu na vifaa vinavyotumia mtandao (Intaneti ). Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Mbeya

 

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Benki ya NBC mara baada ya uzinduzi wa NBC Connect , jukwaa la kidigitali la kisasa linalotoa huduma za benki kwa urahisi na salama, wakati wowote na mahali popote kwa kutumia simu na vifaa vinavyotumia mtandao (Intaneti ). Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika jijini Mbeya

MBEYA Mei 1, 2023: Benki ya Taifa ya Biashara ya (NBC) imezindua huduma ya NBC Connect, ikiwa ni ingizo jipya la huduma za kibunifu za kidijitali katika mkoa wa Mbeya.

Huduma hiyo ya kisasa ya kidigitali inalenga kuwezesha huduma mbalimbali salama za kibenki na ambazo huweza kufanyika sehemu yoyote, muda wowote kwa kutumia simu ya mkononi na vifaa vingine vinavyotumia Intaneti kwa mujibu wa Mkurugenzi wa wateja wakubwa wa benki hiyo, Bw. James Metairon.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijiji Mbeya, Bw Metairon alibainisha kuwa kupitia NBC Connect, wateja wa mkoa huo na maeneo ya  jirani watapata fursa ya kuwa na uwezo wa kufanya miamala yao ya kifedha kwa urahisi zaidi na kupata uzoefu  mpya katika kupata huduma za kibenki.

“Huduma  hii itawapa wateja wetu uwezo wa kufanya aina zote za malipo ikiwa ni pamoja na malipo ya ndani na nje ya nchi, malipo ya Serikali pamoja na malipo kwa mitandao mbali mbali ya simu za mkononi kwa kutumia simu kompyuta, au simu zao za mkononi. Wateja pia wataweza kupata mwenendo wa miamala waliyofanya popote pale walipo pasipo kulazimika kwenda benki.’’ Alisema,

Kwa mujibu wa Bw Metairon, NBC Connect imetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa na yenye usalama wa hali ya juu ambayo imezibngatia na kutoa kipaumbele kwenye usiri wa taarifa za mteja. Ubunifu wa huduma hiyo kuhakikisha taarifa za kifedha za wateja zinalindwa wakati wote.

“Tunafuraha kutambulisha NBC Connect kwa wakazi wa Mbeya na maeneo ya jirani. Mfumo huu wa kibenki wa kidijitali ni uthibitisho wa dhamira ya kuwapatia wateja wetu huduma  bora za kibenki ambazo ni rahisi, salama, na zinazofaa na kukidhi mahitaji ya wateja. NBC Connect itawawezesha wateja wetu kufanya huduma zakibenki popote pale, wakati wowote, na kufurahia huduma hizo bila matatizo.” aliongeza
Pamoja na huduma rahisi na za kisasa, ujio wa huduma hiyo unatajwa kuwa utatoa usaidizi wa binafsi kwa wateja kupitia vituo vyao vya huduma kwa wateja ambapo kupitia mameneja katika vituo hivyo watawasaidia wateja kulingana na mahitaji yao na pia kutoa mwongozo wa jinsi ya kutumia jukwaa hilo kwa ufanisi.

Ili kusherehekea uzinduzi wahuduma hiyo jijini Mbeya, Benki hiyo ilitumia uzinduzi huo kutoa maelezo ya kina juu ya huduma hiyo kwa wateja waliokuwa tayari kujiunga na huduma hiyo ili kuwapa uelewa mpana wa namna ya kuitumia na kufurahia huduma hiyo.

“Tunawaalika wateja wetu wote wa Mbeya na maeneo ya jirani  wajionee urahisi na usalama wa NBC Connect. Ni huduma ambayo inaleta mapinduzi mapya katika namna ambavyo huduma za kibenki zinatolewa. Tuna uhakika  kuwa wateja wetu watufaika nayo kwa kiasi kikubwa , “aliongeza Bw Metairon.
Akiwa katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bw  Benno Malisa aliishukuru Benki ya NBC kwa ubunifu wao mzuri na kuwahimiza wateja kutumia mfumo huo mpya wa kibenki ili kurahisisha shughuli zao za kila siku.

Zaidi, Bw Malisa aliushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kuongeza tawi jingine katika mji wa Mbeya na kwa shughuli zake za uwajibikaji kwa jamii ambazo utoa mchango mkubwa kwa wananchi wengi nchini kote.

ADVERTISEMENT

“Uzinduzi wa NBC Connect jijini Mbeya unawakilisha mpango mkakati wa upanuzi wa benki ya NBC ili kuwafikia wananchi wengi zaidi  na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.’’ Alisema.

Bw Malisa alionyesha kuguswa zaidi na dhamira kubwa ya benki hiyo katika kuwajibika kwa jamii kupitia mipango mbalimbali, kama vile Mbio za Kimataifa za NBC Dodoma zinazohamasisha na kutibu saratani ya shingo ya kizazi, msaada wa afya ya uzazi kupitia kliniki zinazotembea, programu za elimu ya kifedha, uwezeshaji wa vijana.

“Kupitia udhamini wa Ligi Kuu ya NBC mbali na kuongeza ubora wa ligi yetu na kuongeza burudani kwa watanzania udhamini huo umeongeza fursa za ajira kwa vijana na maofisa wengine wengi wa vilabu husika. Hakika napongeza juhudi hizi zinazofanywa na NBC” alisema Bw Malisa.

Uzinduzi wa NBC Connect jijini Mbeya unakwenda sambamba na uzinduzi wa tawi jipya lililofunguliwa katika soko la Mwanjelwa litakalotoa bidhaa na huduma mbalimbali za kibenki, zikiwemo akaunti binafsi na za biashara, mikopo, akiba na uwekezaji, huduma za fedha za kigeni na kidijitali. Wateja pia watapata wataalam wenye uzoefu wa benki ambao wamejitolea kutoa huduma za kibenki za kibinafsi na zenye ufanisi ili kukidhi mahitaji ya kifedha ya jamii.

 

 

Related

Tags: NBC
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KWA FAMILIA YA MMILIKI WA PRECISION AIR
HABARI

RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KWA FAMILIA YA MMILIKI WA PRECISION AIR

by ALFRED MTEWELE
Jun 10, 2023
BREAKING; MMILIKI WA PRECISION AIR AFARIKI DUNIA
HABARI

BREAKING; MMILIKI WA PRECISION AIR AFARIKI DUNIA

by ALFRED MTEWELE
Jun 10, 2023
YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 10, 2023
HABARI

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 10, 2023

by ALFRED MTEWELE
Jun 10, 2023
Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga
HABARI

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

by I am Krantz
Jun 10, 2023
Relationship Manager; Mass Affluent (Acquisition) Job Vacancy at NMB Bank PLC
HABARI

Relationship Manager; Mass Affluent (Acquisition) Job Vacancy at NMB Bank PLC

by ALFRED MTEWELE
Jun 9, 2023
Application Support Specialist Job Vacancy at NBC
HABARI

Application Support Specialist Job Vacancy at NBC

by ALFRED MTEWELE
Jun 9, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2023
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In