Wachezaji wa Marumo Gallants FC ya hapa Afrika Kusini wamegoma kufanya mazoezi leo baada ya kuwa wanadai malimbikizo ya Posho[Bonus] za Mshindano ya CAF.
Wachezaji wa Marumo Gallants FC inaelezwa hata mchezo wao dhidi ya Pyramids FC ya Egypt waligoma ila viongozi waliwaahidi watawapa ambapo hawajalipwa mpaka sasa.
Kikosi cha Marumo Gallants FC kilitarajiwa kufanya mazoezi leo mchana wa saa saba [13:00] kwa hapa Afrika Kusini kwenye uwanja wa Royal Bafokeng.
Marumo Gallants FC wanadai Bonus za Mashindano ya CAF Confederation Cup ndizo ambazo hawajalipwa mpaka sasa.