Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, jijini Dar es Salaam wameanza mgomo leo Mei 15, 2023 wakishinikiza kutatuliwa kwa kero mbalimbali ikiwepo kamatakamata, urasimu bandarini, tozo mbalimbali za biashara zao na madai mengine.
Tayari Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala amefika eneo hilo na kukutana na viongozi wa wafanyabiashara hao, ambapo hata hivyo wameshinikiza wanataka kuonana na Rais Samia Suluhu Hassan ili wamueleze kilio chao.