
Mke wa Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter, Bi. Rosalynn Carter amegundulika kuwa na ugonjwa unaoathiri uwezo wa akili kufikiri, kutunza kukumbuku na kufanya maamuzi ( Dementia).
Familia ya Carter imetoa taarifa hiyo kuhusu Bi. Carter (95) kukumbwa na changamoto hio na kusema, kuwa hawatarajii kutoa maoni mengine juu ya suala hilo.
Wakati mumewe akiwa Rais , Bi.Carter alifanya harakati kadhaa kuhusu masuala ya afya ya akili ikiwemo kuunda tume ya Rais, jambo ambalo linaendelea hadi sasa.
Hivi karibuni mjukuu mmoja wa Rais Carter alinukuliwa akisema “wanaelekea mwisho, babu atatimiza miaka 99 mwezi Oktoba, ni vyema wao kukaa pamoja katika siku hizi za mwisho. Wamekuwa pamoja kwa miaka zaidi ya 70.” Alisema Jason Carter.