ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, June 5, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Mradi Mpya wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabia Nchi – SUSTAIN Eco Wazinduliwa

Dar es Salaam

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
May 24, 2023
in HABARI
0
Mradi Mpya wa  Kuhimili Mabadiliko ya Tabia Nchi – SUSTAIN Eco Wazinduliwa
0
SHARES
23
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

WAZIRI MCHENGERWA ATOA OFA HII BABU KUBWA KUIPONGEZA YANGA

WAZIRI MCHENGERWA ATOA OFA HII BABU KUBWA KUIPONGEZA YANGA

Jun 5, 2023

SIMBA SC IMEWAHI KUCHEZA FAINALI CAF 1993

Jun 5, 2023

KARIM BENZEMA KUONDOKA RASMI MADRID BAADA YA KUICHEZEA KWA MISIMU 14, BERNABEU

Jun 4, 2023
Load More
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1 na jukwaa
Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais, akiwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Muungano, Bw Abdalah Mitawi amezindua Mradi wa SUSTAIN Eco, mradi unaosimamiwa na Taasisi ya international Union for Conservation of Nature ( IUCN) Mkoani Mbeya.
Mradi huo ambao unafadhiliwa na Serikali ya Sweden una thamani ya Dola za Kimarekani 4.5 milioni ambazo ni sawa na Swedish Krona(SEK) 50 milioni.Mradi huu utahusika na usimamizi shirikishi wa ikolojia katika masuala ya Serikali, biashara na jamii husika ,ili kuleta uwiano katika vipaumbele na ukuzi endelevu
Akizungumza Mkuu wa IUCN Eastern & Southern Africa Regional Office Bw. Charlws Oluchina, ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuonyesha ushirikiano mzuri katika Usimamizi wa masuala ya mazingira, aidha ameishukuru Serikali ya Sweden kwa kufadhili masuala ya mazingira na hasa mradi wa SUSTAIN Eco ambao Serikali hiyo imetoa Swedish Krona milioni hamsini.
“Fedha hizi zitasaidia katika kubadilisha, Kuhabarisha, kuimarisha matumizi ya rasilimali na kuzifanya ziwe endelevu.Kwani Usimamizi wa mazingira, bioanuai na mabadiliko ya Tabianchi ni suala endelevu. Tarehe 22/5/2023 ilikuwa siku ya Bionuai Duniani, hivyo uzinduzi wa mradi huu umefanyika kwa wakati muafaka” amesema Bw. Olunuchi.
Nae,Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi. Charlotte Ozaki Macias, amesema kuwa mwaka huu 2023, Serikali ya Sweden inaadhisha miaka 60 ya ushirikiano pamoja na Serikali ya Tanzania
Pamoja na kwamba 22/5/2023 ilikuwa siku ya maadhimisho ya bionuai bado kuwekuwa na ongezeko la jangwa, upungufu wa maji,wanyama na viumbe vingine vinazidi kupungua.
Ongezeko la watu duniani nalo, limechangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya Tabia nchi. Hivyo tuna safari ndefu sana ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi.Amesisitiza Balozi Charlotte.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Mitawi amesema kuwa, kumekuwa na upotevu wa hecta 490 za misitu kila mwaka.Aidha kumekuwa na ongezeko la upungufu wa maji, Upungufu wa chakula na ongezeko la jangwa.
Shukrani kwa Serikali ya Sweden kwa kuonyesha ushirikiano katika kuyajali mazingira. Shukrani pia kwa IUCN kwa kuyajali mazingira na kujishughulisha na masuala ya mazingira.
Tanzania imekuwa ikiathiriwa na kutokuwepo kwa usawa wa bionuai na hasa suala la ukataji wa miti ambapo kila mwaka tunapoteza zaidi ya hekta 490
za miti, na hivyo kuwa na ugomvi kati ya makundi mbalimbali sababu ya kukosa uwiano. Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa sera ya Mazingira.
Aidha Naibu Katibu Mkuu Mitawi amewataka wadau wengine kujihusisha na masuala ya Mazingira kwani uhai wa Binadamu na Viumbe vingine vyote unategemea mazingira.
Nae Mwakilishi wa Taasisi ya IUCN Tanzania ambaye pia Meneja wa Program ya SUSTAIN ECo, Bw. Anthony Mhagama ameeleza kuwa Mradi wa SUSTAIN Eco ambao unasimamiwa na IUCN, Utafanya kazi kwa kushirikiana na African Wildlife Foundation(AWF)pamoja na SNV. Mradi huo utafanya kazi Tanzania katika maeneo matatu ambayo ni Kilombero,Katavi na Morogoro.
Uzinduzi wa mradi wa SUSTAIN Eco ulienda sambamba na mjadala wa masuala ya mazinga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, SAGGOT, NLUPC, Mwakilishi wa RAS Katavi pamoja na mnufaika wa Miradi ya IUCN.
Inaweza kuwa picha ya Watu 12, meza na jukwaa
Inaweza kuwa picha ya Watu 7, jukwaa na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1, miwani na maandishi
Inaweza kuwa picha ya Watu 5, jukwaa na maandishi
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: Dar es SalaamIKULU MAWASILIANOMamlaka ya hali ya hewamradi wa kuhimili tabianchiRais SamiaSWEDEN
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

WAZIRI MCHENGERWA ATOA OFA HII BABU KUBWA KUIPONGEZA YANGA
HABARI

WAZIRI MCHENGERWA ATOA OFA HII BABU KUBWA KUIPONGEZA YANGA

by ALFRED MTEWELE
Jun 5, 2023
MAKAMU WA RAIS AONGOZA ZOEZI LA USAFI SOKO LA MACHINGA DODOMA, NEMC YAACHIWA MAAGIZO HAYA
HABARI

MAKAMU WA RAIS AONGOZA ZOEZI LA USAFI SOKO LA MACHINGA DODOMA, NEMC YAACHIWA MAAGIZO HAYA

by ALFRED MTEWELE
Jun 5, 2023
KUNANI MAGAZETINI LEO JUMANNE TAREHE 22 JUNI
HABARI

KURASA ZA MAGAZETINI LEO JUMATATU TAREHE 05 JUNI 2023

by I am Krantz
Jun 5, 2023
UJUE MPANGO MPYA WA VITUO VYA KUCHAJI MAGARI YA UMEME NCHINI
HABARI

UJUE MPANGO MPYA WA VITUO VYA KUCHAJI MAGARI YA UMEME NCHINI

by ALFRED MTEWELE
Jun 4, 2023
Rais Samia Apunguza Tozo Ya Mafuta
HABARI

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan awaalika Yanga kwa chakula cha jioni kesho Jumatatu

by I am Krantz
Jun 4, 2023
166 New Job Vacancies at TANAPA
HABARI

166 New Job Vacancies at TANAPA

by ALFRED MTEWELE
Jun 4, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2023
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In