
Akiongea wakati wa Mkutano na Wadau wa Mazingira Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka amesema sheria hiyo inasema maeneo ambayo yanazunguka maeneo ya Watu na kuna biashara kelele zinatakiwa kuwa 60 DBA wakati wa mchana na 40 usiku na kwamba sio mara ya kwanza kuwaonya hawa ambao wamefungiwa “Tulishawapa fomu za kuwaonya wengine tuliwaadhibu kwa kuwapa faini lakini waliendelea kukaidi na kukaidi, wamefungiwa siku 14 na watalipa faini ya Tsh. Milioni 5”
“Baadhi ya wale sugu ambao tumeshughulika nao tangu mwanzo na mpaka sasa wanaendelea kutusumbua, kuna Boardroom wa Wilaya ya Kinondoni, kuna Wavuvi Camp, Warehouse, Kitambaa Cheupe, Elements, Soweto, Liquid , kule Dodoma kuna Chako ni Chako, Rainbow, Gentleman, kule Mwanza kuna Kasiki”
“Hawa tumechukua hatua hizo za kufunga kwasababu sio mara ya kwanza kuwaonya tulishapita mara nyingi lakini hawakusikia, baada ya kuwafungia wengi wamefika kuomba msamaha na wengine wameomba wafunguliwe”