Mwanamziki wa miondoko ya Hiphop Professor Jay (Joseph Haule) kupitia ukurasa wa Mtandao wa kijamii wa Insatagram amewashukuru Wasanii wenzake kwa kujitokeza kumjulia hali baada ya siku chache kujipost akiwa nyumbani na kueleza kuwa anaendelea salama na kuwashukuru wote walimsaidia kupambania afya yake kiujumla.
“Leo nimefurahi sana kutembelewa na ndugu zangu wa ukweli @therealfidq @aytanzania @ngomanagwa na @tharealsimplex Asanteni sana kwa kuja, Mungu awabariki sana” ameandika Professor Jay