Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga kwa kutinga hatua ya Fainali Michuano ya Kombe la Shirikisho CAF na kuahidi tena kwa mara nyingine kuwa kila Goli litakalopatikana katika mchezo wa Fainali, atalipia Tsh. Milioni 20.
Rais Samia ameeleza hayo leo Mei 18, 2023 wakati akishiriki uzinduzi wa Mradi wa Minara ya kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini, DDT ya Kampuni ya Azam Media Ltd, Tabata, Jijini Dar es Salaam ambapo yeye aliwasili nafasi ya mgeni rasmi.
Aidha ameongezea kwa kusema atatoa Ndege ambayo itawabeba Timu ya Tanga, wadau na mashaki zake watakaopanga kwenda kushiriki katrika mechi husika.