Rais Dkt. Samia Suluhu ameeleza kuwa baada ya kukamilisha ratiba ya mkutano wa Dharura wa Wakuu wa nchi na Serikali ya Maendeleo Kusini mwa Afrika alipata wasa wa kukutana na Kuuzungumza na Watanzania waishio nchini Msumbiji huku daadhi wkiwa na familia zao.
Aidha amegusia wakiwa kama watanzania wengine waishio kwingineko hapa duniani wamekuwa na mchango mkubwa ktaika kusaidia ndugu na jamaa kupitia pesa wanazozitumia.
“Baada ya kuhitimisha Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika Jijini Windhoek nchini Namibia, nilipata wasaa wa kuzungumza na sehemu ya Watanzania waishio nchini humo, baadhi wakiwa na familia zao. Ndugu zetu hawa kama walivyo Watanzania wengine waishio kwenye maeneo mbalimbali duniani wamekuwa na mchango mkubwa kwa nchi yetu kupitia fedha wanazotuma nchini kusaidia ndugu na jamaa (zaidi ya shilingi trilioni 2.5 kwa mwaka jana), na uwekezaji katika maeneo mbalimbali”. #Repost @samia_suluhu_hassan