Rais Samia Suluhu Hassan amamuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhakikisha anasimamia madai ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na tatizo la waajiri kutowasilisha michango ya Wafanyakazi wao.
–
Akizungumzia kuhusu Bima ya Afya Rais Samia amemuagiza Waziri Mkuu Majaliwa kusimamia madai ya watoa huduma yanayopaswa kulipwa ndani ya siku 60 tangu kupokelewa kama inavyosema sheria ya Bima ya Afya sura ya 395.
–
“Kama mtu alijilimbikizia, ndani ya siku 60 alipe malimbikizo yote, wafanyakazi wafaidike na bima zao za afya.” Amesema Rais Samia
–
Kufuatia tatizo la waajiri kutowasilisha michango ya Wafanyakazi wao,
Waziri Mkuu ataitisha kikao na waajiri ili kumaliza tatizo la hilo.
–
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo mkoani Morogoro, alipokuwa akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT