Timu ya Ruvu Shooting imeshuka daraja rasmi kutoka ligi kuu hadi Championship (ligi daraja la kwanza) msimu ujao baada ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Simba katika mchezo wake wa 28 msimu huu uliochezwa Azam Complex, Chamazi.
Matokeo hayo yanaifanya Ruvu ibaki na alama zake 20 mkiani mwa msimamo wa ligi ikiwa na mechi mbili mkononi ambazo hata kama itashinda zote, haitaweza kutoka kwenye nafasi mbili za mwisho.
Kwa mantiki hiyo Ruvu Shooting ata akishinda michezo yake yote iliyosalia hataweza kuvuka nafasi mbili za mwisho ambazo kimsingi timu mbili zinazoshika mkia ndizo zitakazo shuka daraja.
Msimu huu Ruvu Shooting amecheza michezo 28 ya Ligi Kuu ya NBC, ameshinda michezo mitano, ametoa sare michezo mitano, na amepoteza michezo 20 huku akiwa amefunga magoli 18 na kufungwa magoli 39.
Hivyo basi, nguvu na juhudi zao zote itabidi zielekezwe kwenye ligi daraja la kwanza (Championship) msimu wa 2023/2024 kutafuta nafasi ya kushiriki tena Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025.
Kila la heri Ruvu Shooting kwenye Championship msimu ujao.