ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, June 2, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

SEKTA YA MADINI KUWAVUTA WATALII NCHINI KUELEKEA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI 2023

Dar es Salaam

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
May 24, 2023
in HABARI
0
SEKTA YA MADINI KUWAVUTA WATALII NCHINI KUELEKEA KONGAMANO LA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI 2023
0
SHARES
22
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

No alt text provided for this image“Niwakaribishe wote katika Kongamano la Uwekezaji katika sekta ya Madini yaani ” Mining & Investment Forum 2023″ na niwahakikishie kwa mwaka huu litakua la kitofauti sana , tunategemea kupokea wageni zaidi ya 2000 kutoka kote duniani na tunataka kufungamanisha sekta ya Madini na Sekta ya Utalii kwa maana wale watakao kuja kwenye kongamano hili washafanya Booking kutembelea vivutio vyetu hapa nchini ”

Hayo yamesemwa jana Mei 23,2023 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Madini Dotto Biteko, kwenye Mkutano na Waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa Kongamano la Uwekezaji katika Sekta ya Madini mwaka 2023, lijulikanalo kama Tanzania ‘Mining & Investiment Forum 2023′ litakalofanyika Octoba 25 hadi 26, Mwaka huu.

RelatedPosts

WAZIRI MCHENGERWA AACHA JUKUMU ZITO KWA MABALOZI KUONGEZA WATALII

WAZIRI MCHENGERWA AACHA JUKUMU ZITO KWA MABALOZI KUONGEZA WATALII

May 19, 2023

TANZANIA IKO TAYARI KUSHIRIKIANA NA CANADA ILI INUFAIKE NA MADINI

May 8, 2023

WIZARA KUANZISHA MINADA NA MAONESHO MADINI YA VITO

May 2, 2023
Load More

Amesema kuwa mkutano huo utahusisha wadau kutoka Mataifa mbalimbali Duniani, lengo ni kujadili masuala mbalimbali ya ukuzaji Sekta ya madini.

Dkt. Biteko ameeleza kuwa Mkutano huo, huwa ukifanyika mwezi Februari kila mwaka tangu mwaka 2020, lakini kwa mwaka huu wamebadilisha kutokana na tarehe hiyo kuwa na majukumu mengine yaliyofanyika katika Mataifa mengine ambapo Tanzania ilishiriki.

“Tumefanya mabadiliko ya tarehe ambapo utafanyika kwa siku mbili Octoba 25 na 26, na utakuwa na utofauti na mikutano mingine ambao unaleta wazungumzaji wengi zaidi kuliko miaka iliopita, na mada zitakazozungumzwa ni nyingi zaidi kuliko miaka mingine.

“Utakuwa na wageni kutoka Serikalini, tutawaalika Mawaziri mbalimbali ambao watakuja. Makampuni makubwa ya uchimbaji Duniani watakuja, wachimbaji wakubwa kutoka Duniani watakuja, lakini wataalamu na watafiti mbalimbali watakuwa pamoja nasi.

ADVERTISEMENT

“Kwa hiyo utakuwa ni mkutano mkubwa ambao utakuwa ni wakujadili mwaswala ya ukuzaji wa Sekta ya Madini kuangalia nanma gani Sekta hii inaweza kuwanufaisha watu na kuwatoa katika umaskini” ameeleza Dkt. Biteko.

Aidha Dkt. Biteko amewakaribisha watu mbalimbali kushiriki pamoja nao kwenye mkutano huo, nakwamba Tanzania imejipanga kikamilifu kuhakikisha mkutano huo unakwenda vizuri na kufika malengo yake.
“Nitoe wito kuwa mkutano huu utakuwa ni wa kipekee na wa aina yake, tunataka kufunganisha Sekta ya Madini na Utalii kwaajili ya mkutano huu, kutakuwa na wageni mbalimbali kutoka nchi mbalimbali Duniani kwenye mkutano huu, wameshatoa oda kwenda kwenye mbuga za wanyama na Zanzibar kwa ajili ya utalii, hivyo hii ni fursa”amesema Dkt.Biteko.

Naye kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maji . Nishati na Madini Zanzibar Bwn. Joseph Kilanga amesema Mkutano huu utaongeza watalii na kuongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Zanzibar na kuongezea kuwa Serikali ya Zanzibar ipo tayari kuwapokea watalii hao.

Aidha Muaandaji wa Mkutano huo Bwn. Abdusamad Abdulrahim amesema Mkutano huo utaleta wawekezaji zaidi ya elfu mbili kutoka Nchi za Nje pamoja na kanda zote za AfrikaNo alt text provided for this imageNo alt text provided for this image

ADVERTISEMENT

Related

Tags: DOTO BITEKOWATALIIWIZARA YA MADINIWIZARA YA UTALII
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 2, 2023
HABARI

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 2, 2023

by ALFRED MTEWELE
Jun 2, 2023
Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2bn/-
HABARI

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2bn/-

by I am Krantz
Jun 2, 2023
SERIKALI YAPOKEA BILIONI 15 KUTOKA UINGEREZA KWAAJILI YA MPANGO WA TASAF
HABARI

SERIKALI YAPOKEA BILIONI 15 KUTOKA UINGEREZA KWAAJILI YA MPANGO WA TASAF

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023
RAIS DK. MWINYI AZINDUA KAMATI YA KUZUIA UDHALILISHAJI ZANZIBAR
HABARI

RAIS DK. MWINYI AZINDUA KAMATI YA KUZUIA UDHALILISHAJI ZANZIBAR

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023
WANAWAKE WAONYWA UNYANYASAJI DHIDI YA WANAUME
HABARI

WANAWAKE WAONYWA UNYANYASAJI DHIDI YA WANAUME

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023
JINSI YA KUSAJILI BIASHARA YAKO
HABARI

JINSI YA KUSAJILI BIASHARA YAKO

by ALFRED MTEWELE
Jun 1, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
May 2023
M T W T F S S
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031  
« Apr   Jun »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In