Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inapenda kuwataarifu vyombo vyote vya habari nchini na umma kwa ujumla kuwa leo tarehe 02/03/2023 imezindua rasmi kampeni kwa jina la “Tuwajibike”. ambayo itakuwa endelevu kuanzia mwezi mei.
MALENGO YA KAMPENI
- kuwakumbusha na kuwasisitiza wauzaji wa bidhaa na watoa huduma nchi nzima kuwajibika kwa kutoa risiti halali ya EFD kila wauzapo bidhaa au kutoa huduma.
- kampeni imelenga kuwakumbusha na kuwahamasisha wanunuzi wa bidhaa na huduma kote nchini kuwajibika kudai risiti halali ya EFD pamoja na kuzikagua ili kujiridhisha kuwa inakidhi vigezo vyote muhimu.
- kufuatilia wa utoaji wa risiti halali za EFD nchi nzima pamoja na kuchukua hatua kwa wauzaji wasiofata sheria katika utoaji wa risiti halali za EFD zikiwemo: Kutotoa risiti ya EFD, Kutoa risiti yenye mapungufu kama kuwa na kiwango cha chini kulingana na thamani ya halisi ya bidhaa au huduma, Kutumia risiti moja ya kushindikiza mizigo, Kufanya biashara ya kuuza risiti pasipokuwa na baishara yeyote.
Risiti halali ya EFD inatakiwa kukidhi vigezo vikuu 4 ambavyo ni Jina la biashara, tarehe halisi ya mauzo, Kiasi halisi cha pesa kilichonunuliwa bidhaa au huduma Jina au TIN ya mnunuzi au vyote kwa pamoja.
Tunapenda kuwakumbusha kuwa adhabu ya mfanyabiashara atakaebainika kutokutoa risiti halali ya EFD au kufanya udanganyifu atatozwa faini ya shilling 3,000,000 mpaka shilling 4,500,000 au kifungo cha kisichozidi miaka 3 au vyote kwa pamoja.
Kwa Mnunuzi atakaebainika kufanya manunuzi bila ya kudai risiti halali ya EFD atatozwa faini ya shillingi 30,000 mpaka 1,500,000.
WITO
Tunapenda kutoa wito kwa wafanyabishara wote kuwajibika kwa kutoa risiti halali za EFD bila ya kushurutishwa na wanunuzi kudai risiti halali za EFD kwa kila manunuzi watakayoyafanya ili kuepuka usumbufu usio wa lazima na wakati huo huo kuisadia serikali kutumiza malengo yake ya kuwaletea wananchi maendeleo na kukuza uchumi wa nchi yetu.
Pamoja Tunajenga Taifa letu,
Imetolewa na,
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi