Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. @DrTedros Adhanom Ghebreyesus ameipongeza Tanzania kwa jududi inazoendelea kufizanya katika kupambana na kudhibiti magonjwa ya mlipuko kuingia na kuenea nchini Tanzania.
Dkt. Tendros amesema hayo kwenye kikao maalum na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Marzui pamoja na viongozi wengine waandamizi wakiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu pamoja na wataalam wengine katika Sekta ya Afya.
Dkt. Tedros ameipongeza Tanzania kwa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Marburg na kwa kushirikiana na WHO katika kuimarisha huduma za uchunguzi na udhibiti dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
“Tunaendelea kuipongeza Tanzania kwa juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali kwa ushirikiano na WHO katika kuwaendeleza kitaaluma wahudumu wa Afya ngazi ya jamii na kukubaliana kwa pamoja kuboresha huduma za afya ngazi ya msingi ili kuweza kudhibiti magonjwa ya mlipuko katika hatua za awali na kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza” amesema Dkt. Tendros. Tanzania imeungana na nchi nyinginezo wanachama wa Umoja wa Mataifa chini ya Shirika la Afya Duniani kushiriki kikao hiki muhimu cha 76 cha Shirika la Afya Duniani kinachofanyika Geneva, Uswisi.