Ikiwa yamesalia masaa machache leo Mei 17, 2023 Yanga SC kuchuana vikali dhidi ya Marumo Gallants katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho huko nchini Afrika Kusini katika Dimba la Royal Bafokeng nchini humo watati ikitakiwa kulinda ushindi wake wa goli 2-0 zilizopatikana wakiwa wenyeji wa mchezo.
Kwa kuwaunganisha Wadau na Mashabiki wa Klabu hio ili kuendelea kuipa nguvu timu hio, Yanga kwa mara nyingine watafunga Big Screen (HAIER HD) katika makao makuu yake ili mashabiki waweze kushuhudia mtanange huo wa kukata na shoka.
Yanga wanatarajia kucheza dhidi ya Marumo Gallants leo saa moja usiku na watahitaji ushindi au sare yoyote ili kuweza kufuzu kucheza fainali ya Kombe la
Shirikisho Barani Afrika kwakuwa wao wana faida ya jumla ya goli (Agg) 2-0 walizopata katika mechi ya raundi ya kwanza Dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.