Leo Klabu ya Yanga SC imeingia kwenye ushirikiano na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam, Ofisi ya Afya ya Mkoa na UNICEF TCO katika jitihada za kuongeza uelewa kuhusu kuzuia na kudhibiti magonjwa ya mlipuko haswa yanayosambazwa kwa maji na vijidudu ikiwemo kipindupindu.
Hayo yamethibitishwa na Mtendaji Mkuu wa klabu hio Andre Ntine hii leo Mei 5 kupitia mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika jijini Dar es Salaam.
“Tunafurahi kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika kampeni ya kuongeza uelewa juu ya magonjwa yote ya kuharisha ikiwa ni pamoja na mlipuko wa kipindupindu. Tunaahidi kusaidia serikali kushughulikia visababishi vyote vya magonjwa ya kuharisha na kutapika katika jiji la Dar es Salaam,” Andre Mtine Mtendaji Mkuu wa Yanga SC.“Ushirikiano na Yanga ni mfano wa jinsi ushirikiano kati ya wadau tofauti unavyoweza kucheza jukumu muhimu katika kukabiliana na changamoto za afya ya umma. Tunafurahi kushirikiana na Yanga tena, kwani ushirikiano wetu wa awali kwenye Uviko ulifana sana. Tunatumaini kufikia watu wengi iwezekanavyo” Dkt Rashid Mfaume, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
“Kitendo cha Serikali kutuamini na kutukabidhi kampeni hii ya kupambana na kipindupindu basi inaonesha ukubwa wa klabu hii. Nasi kupitia matawi yetu tutahamasisha wanachama wetu kusambaza elimu dhidi ya magonjwa yote ya mlipuko” Haji Mfikirwa – Mkurugenzi wa matawi, mashabiki na wanachama.
#ishiKijanja #KingaNiBoraKulikoTiba
#KoncepttvUpdates