Klabu ya Yanga imefuzu nafasi ya kucheza Fainali katika mIchuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAFCC) baada ya kuichapa Marumo Gallants FC kutokea Afrika Kusini kwa jumla ya Goli 4-0 baada ya kuwa na faida ya Goli 2 walizopata ushindi nyumbani hhku mpinzani wake huyo akiwa ndio mwenyeji wa mchezo huo hapo jana nakufanya Bendera ya Nchi ya Tanzania iendelee kupepea kimataifa kupitia uwakilishi wao.
Yanga ilishinda Goli 2-0 katika mchezo uliochezwa Mei 10 katika Dimba la Mkapa hapa jijini Dar es Salaam.
Hakika historia imendikwa kwa klabu hio kutokea nchini Tanzania kuweza kutinga hatua ya kucheza Fainali Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika hakika ni furaha kwao, wadau wa soka na mashabiki kiujumla kuchuhudia makubwa yakifanywa msimu huu.

