ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, September 23, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

DAWASA, BONDE LA WAMI/RUVU WAAINISHA MIKAKATI UTUNZAJI VYANZO VYA MAJI

Dar es Salaam.

MTEWELE ALFRED by MTEWELE ALFRED
Jun 2, 2023
in HABARI
0
DAWASA, BONDE LA WAMI/RUVU WAAINISHA MIKAKATI UTUNZAJI VYANZO VYA MAJI
0
SHARES
102
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

No alt text provided for this imageNa Crispin Gerald,

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeelezea nia ya kuendelea kuongeza vyanzo vya uzalishaji maji ikiwemo maji ya ardhini ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya wananchi wa Dar es Salaam na Pwani, sambamba na kudhibiti uharibifu na uchafuzi wa maji.

RelatedPosts

MAHAKAMA KUU YAMWAMURU BOCCO KULIPWA MILIONI 200 KWA MATUMIZI YA PICHA YAKE

MAHAKAMA KUU YAMWAMURU BOCCO KULIPWA MILIONI 200 KWA MATUMIZI YA PICHA YAKE

Sep 7, 2023

BENKI YA NBC YAZINDUA LOGO MPYA YA LIGI LA CHAMPIONSHIP

Sep 7, 2023

KITAPIGWA HAPA ALGERIA NA TAIFA STARS

Sep 6, 2023
Load More

Hii ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa maji kupitia visima virefu pamoja na ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha maji la Kidunda, pamoja na ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha maji wa Rufiji.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Ndugu Laston Msongole wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa Wami/Ruvu kwenye mradi wa maji Kigamboni uliotekelezwa na DAWASA.

Amesema kuwa katika kukabiliana na mahitaji ya maji ya wananchi, Mamlaka inaendelea na kazi ya uchimbaji wa visima virefu zaidi kwenye Wilaya ya Kigamboni na kazi ya utafiti kubaini maeneo mengine yenye hazina ya maji ya ardhini yanayofaa kuhudumia wananchi.

“Tunashirikiana na Bonde la Wami/Ruvu katika kutafiti na kutunza vyanzo vya maji ya ardhini ambayo yameonekana yanaweza kutoa huduma kwa wananchi kwa zaidi ya miaka hamsini ijayo,” ameeleza.

Ameongeza kuwa kwa sasa mradi wa maji Kigamboni unazalisha lita milioni 70 kwa siku kutoka kwenye visima virefu 7 vilivyokamilika, ambapo wakazi wa Temeke, Chang’ombe na Kinondoni, na mpango uliopo ni kufikisha maji kwenye jimbo la Ukonga.

“Tayari zoezi la maunganisho ya maji kwa wateja limeanza, ambapo wateja 7,000 wameshaunganishwa na kazi inaendelea kufikia wananchi takribani 128,000 wa Kigamboni,” ameeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Elibariki Mmasi amesema kuwa Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana na DAWASA tunaendelea kufanya tafiti kwenye maeneo oevu ili kuhakikisha maji yaliyomo yanahifadhiwa na yaweze kutumika kutoa huduma kwa wananchi.

“Huu ni mkakati madhubuti wa kuhakikisha tunaongeza uzalishaji wa majisafi kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo maji ya ardhini ili miradi ya maji ambayo Serikali inawekeza fedha nyingi iweze kuleta tija kwa jamii inayokusudiwa,” ameeleza Mhandisi Mmasi.

Mbali na hapo tumejipanga na tunaendelea na jitihada za kudhibiti shughuli za kibadamu zinazofanywa kwenye safu za milima ya Uluguru inayotoa maji ya chemchem na maeneo ya mito inalindwa kikamilifu.

No alt text provided for this imageZiara ya Wajumbe wa Bodi ya Wami/Ruvu kwenye mradi wa maji Kigamboni imeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bi Hafsa Mtasiwa.No alt text provided for this imageNo alt text provided for this imageNo alt text provided for this image

 

 

Related

Tags: Dar es SalaamDAWASARUVUWAMIWIZARA YA MAJI
MTEWELE ALFRED

MTEWELE ALFRED

Related Posts

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy
BIASHARA

Maurel and Prom: Empowering Tanzania’s Sustainable Energy Economy

by I am Krantz
Sep 22, 2023
DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA
HABARI

DR KONGO YATAKA MONUSCO KUONDOKA HARAKA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA
HABARI

HAIER TANZANIA NA AZAM TV WAUNGANA KUKIWASHA KWA PAMOJA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
MNH YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA TUNDU DOGO MOJA
AFYA

MNH YAFANYA UPASUAJI WA KWANZA TUNDU DOGO MOJA

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
SBL KUUNGANISHA TAMADUNI KUPITIA OKTOBA FEST
HABARI

SBL KUUNGANISHA TAMADUNI KUPITIA OKTOBA FEST

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023
TAWA YATAKIWA KUJIPANGA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO
HABARI

TAWA YATAKIWA KUJIPANGA KUONGEZA UKUSANYAJI MAPATO

by SUZO SHUKRANI
Sep 21, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

June 2023
M T W T F S S
 1234
567891011
12131415161718
19202122232425
2627282930  
« May   Jul »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In