Nyota wa Soka kutokea nchini Ufaransa Karim Benzema ametambulishwa rasmi ndani ya Klabu ya Al-Ittihad baada ya siku chache awali kusaini mkataba wa makubaliano ya kuitumikia klabu hio kwa dili la miaka mitatu, akiwa na mshahara wa Euro 200m kwa msimu.
Benzema amejiunga na klabu hi akitokea klabu ya Real madrid ambayo ameitumikia kwa misimu 14 tangu aungane nayo mwaka 2009 akiwa bado ana umri wa miaka 21.